TBL KUMENOGA TUKUTANE BAA!

SHINDA GARI KILA MWEZI

Tafadhali weka namba yako ya simu kabla ya kuwasilisha

Tafadhali weka code yako kabla ya kuwasilisha
Tafadhali jaza jina lako kamili kabla ya kuwasilisha
Tafadhali chagua jinsia yako kabla ya kuwasilisha
Tafadhali weka tarehe ya kuzaliwa iliosahihi
Tafadhali chagua mwezi uliozaliwa kabla ya kuwasilisha
Tafadhali weka mwaka sahihi uliozaliwa
Tafadhali chagua mkoa kabla ya kuwasilisha

Tafadhali kubali vigezo na masharti kabla ya kuwasilisha
Tafadhali kubali vigezo na masharti kabla ya kuwasilisha
Tafadhali weka code yako kabla ya kuwasilisha

Vigezo na masharti ya promosheni ya “TBL Kumenoga”

 1. Promosheni hii itaanza Septemba 15, 2018 na kumalizika Novemba 30, 2018. Maombi yatakayoletwa baada ya hapo hayatakubaliwa.
 2. Shindano hili ni kwa wakazi wote wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania isipokuwa wafanyakazi wa Tanzania Breweries Ltd (TBL) pamoja na wakala wao wa Matangazo, PR, familia na ndugu, Washauri, Wakurugenzi, Washirika pamoja na washirika wa kibiashara ya waliotajwa hapo juu.
 3. Washiriki wote wanatakiwa kuwa na umri zaidi ya miaka 18 siku ya kuwasilisha maombi. Washindi watatakiwa kuonyesha vitambulisho halali kama ushahidi wa utambulisho.
 4. Ili kuingia kwenye shindano, mshiriki atatakiwa kununua muunganiko wa chupa 3 za aidha Kilimanjaro Premium Lager, Safari Lager, Balimi Extra Lager za 500ml au Castle Lite za 375ml ili kupata kuponi yenye namba ya kipekee. Mshiriki atatuma namba iliyo kwenye kuponi kwenda 15451 na kuingia kwenye droo ya kushinda gari moja kwa moja. Gharama za SMS za kawaida zitatozwa na vifurushi havitatumika.
 5. Kwa kukubali kushiriki, washiriki wote wanakubaliana na vigezo na masharti yaliyotajwa.
 6. Washiriki watapata nafasi ya kushinda gari moja (1) kila mwezi; ambayo ni gari moja (1) kwa mshindi mmoja ambaye atakabidhiwa gari hilo katika kiwanda cha TBL kilicho karibu yake mwezi mmoja baada ya kushinda.
 7. Vigezo vya ushindi vitategemea na ushiriki wa mara nyingi na namba zitachaguliwa kwa mfumo wa kompyuta na kuingizwa kwenye droo.
 8. Mshindi atapigiwa simu mara 3 kwenye namba aliyotoa kupitia ushiriki. Iwapo hatapokea baada ya mara 3, droo itaendeshwa upya kumpata mshindi mwingine.
 9. Iwapo mshindi hatapatikana kwenye simu yake kwa muda wa siku 3 mfululizo baada ya droo, zawadi itarudishwa kwa promota kwa ajili ya kutafuta mshindi mwingine.
 10. Kutakuwa na zawadi za papo hapo kwenye baa zilizochaguliwa ambazo zitajumuisha Tisheti, kofia, bia za bure pamoja na nyinginezo.
 11. Washindi wa zawadi za papo hapo watakabidhiwa zawadi zao papo hapo kwenye baa zenye promosheni na wataamuliwa na promota.
 12. Si Tanzania Breweries Ltd wala wakala wake wa matangazo, urushaji na PR, au washirika wao wa kibiashara watahusika kwa njia moja ama nyingine kwa upotevu, uharibifu au gharama zitakazotokea kwa mshiriki wa droo kwa zawadi husika.
 13. Vigezo na masharti haya yanaratibiwa na sheria za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na washiriki wanakubaliana kuhusika moja kwa moja na utaratibu wa Mahakama.
 14. Washindi wanaweza kutakiwa kushiriki kwenye matangazo yanayohusiana na promosheni hii, na hivyo wanawajibika kukubaliana na hili. Washindi hawatakuwa na haki ya malipo au marupurupu kwenye matangazo haya. Matangazo haya pamoja na viambatanisho vyake vyote vitakuwa ni mali ya Tanzania Breweries Ltd na wawakilishi wake.
 15. Mwakilishi wa Tanzania Breweries Ltd ana haki ya kubatilisha au kusitisha kwa muda shindano hili iwapo kutatokea sababu zitazopelekea kufanya hivyo.
 16. Tanzania Breweries Ltd pamoja na wakala wake hawatahusika na usumbufu utakaotokea wakati wa kuwasilisha maombi ya kushiriki kwenye shindano hili.
 

JISHINDIE MILIONI

Tafadhali weka code yako kabla ya kuwasilisha